Tuesday, August 8, 2017

8 August 2017, Mitandao ya kijamii yafungwa nchini DR Congo

Serikali ya DR Congo imetoa amri ya kufungwa kwa mitandao yote ya kijamii ili kuzuia usambazaji wa picha na video za ghasia zinazoendelea.

Aidha hatua hiyo imechukuliwa kufuatia ongezeko la upinzani dhidi ya rais Joseph Kabila ambaye amekataa kujiondoa madarakani wakati awamu yake inamalizika mwezi Desemba .

Migomo ya kitaifa imepangwa kufanyika Jumanne na Jumatano .
Mapigano ya Jumatatu baina ya kundi la Bundu dia Kongo na vikosi vya usalama ,yalipelekea vifo vya watu 14.

Mkuu wa idara ya mawasiliano nchini humo Oscar Manikunda Musata amefahamisha kwamba mitandao ya kijamii kama Twitter,Whatsap ,Facebook na Instagram itafungwa kwa muda .

No comments: