Mapigano kati ya majeshi ya serikali na wapiganaji wa kundi la Maute lenye uhusiano na kundi la kigaidi la DAESH yamekuwa yakiendelea huku nchi ya Ufilipino ikionyesha juhudi za kuujenga mji wa Marawi ulioharibiwa na mapigano hayo.
Kwa mujibu wa habari,ujenzi wa nyumba 1100 za kwanza unatarajia kuanza katika wiki ya kwanza ya mwezi Septemba.
Ripoti zinaonyesha kuwa nyumba hizo zitajengwa katika eneo la hekta 11 za ardhi ya binafsi kusaidia kuwapa nyumba wale wote waliohama makazi yao wakati wa mapigano hayo.
Ni takriban watu zaidi ya elfu hamsini wameripotiwa kuhama na familia zao wakihofia maisha yao.
Mapigano kati ya wapiganaji wa Maute na serikali yalianza mnamo mwezi Mei 23 baada ya serikali kushindwa kumkamata Isnilon Hapilon anaetambulika kama gaidi anaesakwa Ufilipino nzima.Washington imetoa ofa ya dola milioni tano kwa yeyote atakaemkamata.
Rais Rodrigo Duarte anataka gaidi huyo akamatwe yu mzima au amekufa.
Inasemekana kuwa Hapilon aliyakimbia mapigano hayo ndani ya siku saba za kwanza lakini kuna fununu zinasema kuwa huenda akawa bado Marawi akaiwasaidia magaidi katika mapigano hayo.
Hata hivyo kwa sasa ni vijiji viwili tu vimebaki vikifanya mapigano hayo kwani vijiji vingine vimeshakombolewa.
No comments:
Post a Comment