Monday, August 7, 2017

7 August 2017, Nane wapoteza maisha katika shambulizi la kanisa Nigeria

Watu nane wameripotiwa kufariki na wengine 18 kujerujiwa siku ya Jumapili asubuhi baada ya mwanamume mwenye silaha kuvamia kanisa la wakatoliki kaskazini mwa mji wa Anambra.

Kamishna wa polisi wa Anambra,Garba Umar amevielezea vyombo vya habari jinsi tukio lilivyotokea.

Bwana Garba amesema kuwa mwanamume aliyefanya shambulizi hilo aliongea lugha ya Lgbo.

Kwa mujibu w ahabari,polisi huyo amekataa ripoti zinazosema kuwa shambulizi hilo limefanywa na kundi la kigaidi la Boko Hram.
Ripoti zinaonyesha kuwa aliyefanya shambulizi hilo ni mzaliwa wa pale pale na sio mtu kutoka nje.

Mwanamume huyo alivamia kanisa hilo majira ya saa kumi na mbili wakati waumini wakifanya misa ya asubuhi,akiwa amevaa nguo nyeusi na kuanza kufyatua risasi.

Baada ya mwanamume huyo kuwapiga risasi wale aliyokuwa amewalenga alianza kufyatua risasi ovyo na kujeruhi waumini wengi.

Vilevile inasemekana baada ya shambulizi kutokea,viongozi wa juu wa sehemu hiyo walianza kutokubaliana.

No comments: