Wednesday, August 2, 2017

2 August 2017, Neymar kujiunga na PSG kwa kitita cha £198m

Nyota wa Barcelona Neymar amepewa ruhusa ya kuondoka Barcelona akitarajiwa kujiunga na PSG katika kitita cha rekodi ya pauni milioni 198.

Raia huyo wa Brazil amewaambia wachezaji wenzake wakati wa mazoezi siku ya Jumatano kwamba angependa kuondoka.

Alipewa ruhusa na meneja Ernesto Valvarde asifanye mazoezi na badala yake kushughulikia mpango wa uhamisho wake.

No comments: