Monday, August 14, 2017

14 August 2017, Raila Odinga awatolea wito wafuasi wake kususia kazi Jumatatu Kenya

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga wawatolea wito wafuasi wake kususia kazi Jumatatu
Raila Odinga, kiongozi wa upinzani katika uchaguzi mkuu nchini Kenya amewatolea wito wafuasia wake kutowasili kazini jumatatu.

Wito huo wa kususia kazi ni kwa ajili ya kupinga matokea ya uchaguzi yaliotangazwa na tume ya uchaguzi Agosti 12.

Tume ya uchaguzi ilimtangaza rasmi Uhuru Kenyatta kushinda uchaguzi kwa asilimia  54 ya kura.

Raila Odinga amewahutubia wafuasi wake Agosti 13 kwa mara ya kwanza tangu kuanfanyike uchaguzi.

Hutuba hiyo ameitoa katika eneo la Kibera na kuahidi kutoa mikakati yake ifikapo Jumanne.

No comments: