Takriban watu 19 wakiwemo wapiganaji wa Al Shabaab wameuawa na wengine kujeruhiwa vibaya baada ya mapigano kuzuka kusini magharibi mwa Somalia.
Mohammed Hasan Fiqi kiongozi wa sehemu hiyo amesema kuwa mapigano yaliyotokea katika mkoa wa Bakool yamesababisha vifo vya wapiganaji waAl Shabaab 13 na sita wa Abu Mansoor.
Abdirasak Abdi,msaidizi wa waziri wa ulinzi amesema kuwa uongozi wake unlisaidia kundi la al Masoor ili kuweza kulitokomeza kundi la al Shabaab.
Kwa mujibu wa habari,mapigano hayo yalianza baada ya Al Shabaab kuvamia kijiji cha Abal kilicho kilomita 390 kutoka Mogadishu.
Ripoti zinaonyesha kuwan Abu Mansoor kiongozi wa Al Shabaab aliachana na kundi hilo mwaka 2013.
No comments:
Post a Comment