Mahakama moja nchini Misri imetoa adhabu ya kifungo cha maisha kwa watuhumiwa 43 waliohusika na ghasia za 2011 baada ya kuondolewa kwa Hosni Mubarak kufuatia shughuli zake za uasi .
Wakati huo huo mahakama hiyo iliwatoza washutumiwa hao faini ya takriban dola milioni moja .
Vile vile mahakama hiyo imewapa vijana wengine 9 adhabu ya miaka 10 gerezani .
Hata hivyo watuhumiwa hao wana fursa ya kukata rufaa .
Mnamo mwaka 2011 ghasia zilizuka baina ya waandamanaji na vikosi vya usalama na kupelekea vifo vya watu 18 na kadhaa kujeruhiwa
No comments:
Post a Comment