Wednesday, July 26, 2017

26 july 2017, Buhari kutekeleza tena majukumu yake ya urais baada ya ushauri wa daktari

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari anatarajiwa kurejelea majukumu yake kama rais iwapo madaktari wake watapendekeza yeye kufanya hivyo .

Kumekuwa na ripoti zakupingana kuhusu hali ya afya ya rais Buhari mwenye umri wa miaka 74.

Baada ya miezi 3 tangu rais huyo kuanza likizo yake ya matibabu,ofisi yake ilitoa picha yake iliyoonyesha akitabasamu .

Rais Buhari aliondoka Abuja na kuelekea London kwaa ajili ya matibabu Mei 7 mwaka huu .

Mnamo Julai 24 rais Buhari aliandika barua kwaa rais wa Guinea Alpha Conde iliyosoma kuwa;
"Ninaendelea kupata nafuu kila siku na madaktari wakipendekeza kumaliza likizo yangu ya matibabu nitarudia majukumu yangu ya urais mara moja ,nitaendelea kuhudumia wananchi wangu walionichagua na wanaoendelea kuniombea nipone."

Rais Buhari aliingia madarakani Mei 2015 ,kwa sasa Yemi Osinbajo anatekeleza majukumu kwa niaba yake hadi pale atakaporudi ofisini tena 

No comments: