Thursday, May 3, 2018

OMMY DIMPOZ ATISHWA NA UJIO MPYA WA ALIKIBA

Ikiwa ni siku ya pili tangu Ommy Dimpoz  aachie kazi yake mpya 'Yanje' ambayo  ameshirikiana  msanii Seyi Shay kutoka nchini Nigeria, amemuomba msanii Alikiba awahurumie. 
Ommy Dimpoz amesema hayo hivi karibuni  baada ya Alikiba kutangaza rasmi kuwa wimbo huo mpya wa Ommy Dimpoz ukifikisha watazamaji milioni tatu Youtube ataachia  wimbo wake mpya baada ya  Maumivu perday
Baada ya ahadi hiyo ya Alikiba ndipo alipokuja Ommy Dimpoz na kumuuliza Alikiba kama atatoa ngoma zote tano kwa wakati mmoja au ataanza kuachia moja moja, hii ni ishara kwamba tayari kuna nyimbo zaidi ya tano kutoka wa Alikiba ambazo zipo tayari kwa ajili ya kuachiwa. 
Aidha Msanii Alikiba akijibu moja ya swali kutoka kwa shabiki yake kupitia mtandao wa kijamii ambaye alitaka kufahamu kuwa hilo dude ataliamsha lini ndipo alipojibu kuwa anawapa siku 10 tu baada ya hapo anaweza kuachia wimbo wake huo mpya

No comments: