Mtandao rasmi wa Unai Emery umeweka picha iliyo na ujumbe: "Nasikia fahari kuwa katika familia ya Arsenal."
Emery ambaye ni meneja wa zamani wa Paris St-Germain anatarajiwa kuwa rasmi mrithi wa Arsene Wenger wiki hii.
Arsenal bado haijathibitisha kuwa Emery ndiye kocha mpya.
Lakini picha ya Emery iliyoambatana na ujumbe huo na nembo ya Arsenal iliwekwa kabla ya muda mfupi badaye kuondolewa.
Haijulikani kama picha hiyo iliwekwa kimakosa au ni kazi ya wadukuzi.
No comments:
Post a Comment