Rais Dkt John Magufuli amezindua jengo la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PSPF na tawi la benki ya NMB Makao Makuu Dodoma na kuitaka benki hiyo kuangalia upya kiwango cha gawio inayotoa kwa serikali ili iweze kunufaika.
Akizungumza mjini Dodoma wakati wa uzinduzi na ufunguzi wa taasisi hizo Rais Magufuli amesema benki ya NMB imekuwa ikiongeza faida kila mwaka lakini gawio kwa serikali haliridhishi.
Aidha amezipongeza benki zote zinazotoa mikopo kwa wawekezaji wa viwanda mbalimbali nchini.
Takribani miezi 25 imetumika kukamilisha jengo PSPF mjini Dodoma lenye minara miwili mmoja ukiwa na ghorofa 11 na mwingine ghorofa tatu ambalo limegharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 35
ADMIT TBC
No comments:
Post a Comment