Sunday, April 22, 2018

22 APRIL 2018,EMMANUEL MBASHA ,AMFARIJI JOKATE MWIGELO

Siku chache baada  ya msanii Alikiba, kuoa maswali mengi yamekuwa yakitupwa kwa mwanamitindo  Jokate Mwegelo  ambaye inasemekana  awali  alikuwa na mahusiano  ya kimapenzi na Alikiba  ingawa  kila mmoja wao kukana juu ya hilo 

Muimbaji wa nyimbo za Injili nchini, Emmanuel Mbasha amemuelezaJokate kuwa asijali kwa  ndoa inakuja, hata hivyo haijafahamika iwapo ni yao wawili au laa. Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika;

“Usihofu Mungu hajakuacha Jokate Mwegelo yakwetu inakuja, tv zote zitakuwa live ukumbini hadi wasafi tv,” amesema Mbasha.

Katika kuhadhimisha kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa March 20, 2018 Jokate aliweka wazi kuwa yupo mbioni kuolewa ingawa hakuweka wazi ni nani atahusika katika ndoa hiyo.

Pia muimbaji Mbasha kwa sasa hayupo katika ndoa na hii ni baada ya kuachana na aliyekuwa baby mama wake, Madam Flora ambaye aliolewa April 30, 2017 na Daudi Kusekwa.

No comments: