Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva, Nandy amemtupia lawama BillNass na kuwaomba radhi Watanzania wote waliopatwa na mfadhaiko baada ya video hiyo kuvuja kwenye mitandao ya kijamii.
Nandy amesema kuwa video hiyo ni kweli ya kwake na BillNass na walipiga kipindi hicho mwaka 2016 walipokuwa kwenye mahusiano ila ameshangazwa kuona video hiyo waliyopiga wakiwa faragha kuvuja mtandaoni.
Nandy amesema “Nilikuwa na mahusiano na Bill Nass mwaka 2016, na tulikubaliana mimi na yeye mahusiano yetu yawe private sielewi sasa hiyo video imevujaje, au ana maana gani kuitoa namtafuta kwenye simu (Bill Nass) ila simpati hiyo video ni ya zamani ila ni ya private.
Ni video ambayo ilishutiwa zamani mwaka 2016 kwenye Snapchat na baadaye mnarushiana kama mwenzio anaitaka, Siunajua mtu na mpenzi wake mkiwa faragha.
Naomba radhi sana kwa familia yangu, kanisani kwangu, mashabiki serikali yangu kwa kweli video imenichefua sana mpaka hapa ninapoongea nimechefuka, ila adhabu ya maumivu ninayoipata sasa hivi ni kutokana na kumuamini mwenzangu,“amesema #Nandy kwenye mahojiano yake na MCL Digital.
Mapema leo Aprili 12, 2018 video ya Nandy na BillNass wakiwa utupu imevuja kwenye mitandao ya kijamii ikiwaonesha wawili hao wakiwa katika hali ya mahaba kitandani,
No comments:
Post a Comment