Friday, March 30, 2018

30 March 2018,Lewandowski kuhamia Real Madrid

Mshambuliaji wa Bayern Munich Robert Lewandowski, mwenye umri wa miaka 29, atawasilisha maombi yake ya kutaka kuhamia Real Madrid msimu huu wa majira ya joto.

Mchezaji wa Chelsea mwenye umri wa miaka 25 na mchezaji wa kimataifa wa Uhispania Alvaro Morata ni mmoja wa washambuliaji ambao Bayern Munich inamtaka kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Pole iwapo watampoteza. (AS - in Spanish)

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Paris St-Germain midfielder Hatem Ben Arfa ametangaza kuwa ataondoka katika Ligi kuu ya Ufaransa mwisho wa msimu. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31, raia wa Ufaransa, amekuwa na uhusiano na Leicester City. (Sun)

No comments: