Wednesday, March 28, 2018

28 March 2018,Prof,Jay -Kutoacha muziki kamwe

MWANAMUZIKI wa muziki wa waafrika weusi nchini (Hiphop) ambaye pia ni Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule ‘Professor Jay, amefunguka kuwa hataacha muziki kamwe, kwani kufanya hivyo ni sawa na kuwasaliti wananchi wake ambao wamemfahamu na kumpeleka mjengoni kupitia muziki wake alioufanya kwa miaka mingi.

Professor Jay ambaye anajiita mbunge wa binadamu na wanyama kutokana na Hifadhi ya Mbuga ya Mikumi kuwa kwenye jimbo lake, alisema hayo hivi karibuni alipokuwa akitambulisha wimbo wake mpya uitwao Pagamisa ambao amemshirikisha Prodyuza Mr. T Touch.

Prodyuza Mr. T Touch.
“Pagamisa ni kazi nzuri ambayo imepokelewa vizuri na kiukweli miaka yote ya maisha yangu nitaendelea kutoa kazi nzuri na siwezi kamwe kuacha muziki kwani kufanya hivyo ni sawa na kuwasaliti wananchi ambao wamenipeleka mjengoni kupitia muziki huu ambao ninafanya,” alisema Professor Jay.

No comments: