Friday, February 2, 2018

2 February 2018,Algeria Riyad huenda akapigwa faini ya £200,000 kutokana na kususia mazoezi

Winga wa Leicester na Algeria Riyad Mahrez, 26, huenda akapigwa faini ya £200,000 na klabu hiyo iwapo ataendelea kususia mazoezi baada yake kuzuiwa kuhamia Manchester City. (Mirror)

West Ham walishindwa kumnunua mshambuliaji kutoka Algeria Islam Slimani, 29, kwa sababu Leicester walikataa kufanya biashara na Karren Brady baada ya mwenyekiti huyo wa West Ham kunukuliwa gazetini akizungumzia kufutwa kwa meneja wa zamani wa Leicester Claudio Ranieri. Slimani amehamia Newcastle kwa mkopo. (Guardian)

Manchester United wataangazia kumtafuta kiungo wa kati ambaye atamsaidia Mfaransa Paul Pogba, 24 kufikia upeo wake wa uchezaji soko litakapofunguliwa mwisho wa msimu. (Mail)

Arsenal watajaribu tena kumtafuta fowadi Mbrazil Malcom, 20, kutoka Bordeaux majira ya joto, na huenda wakamtafuta pia kipa wa Atletico Madrid kutoka Slovenia Jan Oblak, 25, kutafuta mlinda lango wa kuchukua nafasi ya Petr Cech, 35. (Evening Standard)

No comments: