Mfuko wa Kuhudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) umetangaza kuwa mtoto mmoja wa Kiiraqi kati ya wanne nchini humo anaishi katika hali ya umaskini na kwamba Wairaqi wengine milioni nne wanahitaji msaada ikiwa ni natija ya kujiri vita vya kundi la kigaidi la Daesh huko Iraq.
Unicef imebainisha kuwa taasisi za elimu zimeshambuliwa mara 150 huku wafanyakazi wa vituo vya afya wakishambuliwa mara 50 huko Iraq tangu mwaka 2014 hadi sasa na kwamba nusu ya shule nchini humo zinahitaji kufanyiwa ukarabati.
Ripoti ya Shirika la Unicef imeongeza kuwa watoto wa Kiiraqi milioni tatu walilazimika kukatisha masomo katika miaka hiyo yote.
Garrett Capillar Mkurugenzi wa Kieneo wa Shirika la Unicef katika Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika amewataja watoto hao kuwa ni taifa la kesho huko Iraq na kuzitolea wito nchi mbalimbali kusaidia kuwekeza kwa ajili ya kuwasaidia watoto hao na kuijenga upya Iraq.
Mwezi Disemba mwaka jana iraq ilitangaza kupata ushindi dhidi ya kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh na kukomboa maeneo yote nchini humo yaliyokuwa yakishikiliwa na kundi hilo mwaka 2015 na 2015.
No comments:
Post a Comment