Meneja Mauricio Pochettino aliwasifu sana vijana wake wa Tottenham kwa kuanza mechi kwa ukali baada ya Christian Eriksen kufunga bao sekunde 11 pekee baada ya mechi kuanza, na kufanikiwa kulaza Manchester United 2-0 uwanjani Wembley.
Ilikuwa siku ya miamba kulala kwani mabingwa watetezi Chelsea pia walilazwa 3-0 na Bournemouth, ushindi ambao meneja wao Eddie Howe ameueleza kuwa matokeo bora zaidi kwao Ligi ya Premia.
Mabao ya kipindi cha pili kutoka kwa Callum Wilson, Junior Stanislas na Nathan Ake yaliwahakikishia Bournemouth ushindi wao wa kwanza ugenini katika mechi saba za ligi, Chelsea nao wakaondoka uwanjani na kichapo kilichofikia kipigo kikubwa zaidi walichopokezwa msimu huu
No comments:
Post a Comment