Umoja wa Ulaya wafahamisha Jumatatu kuongeza vikwazo dhidi ya Korea-Kaskazini kufuatia majaribio yake ya makombora ya nyukli.
Korea-Kaskazini licha ya kukabiliwa na vikwazo imekuwa ikifanya majaribio ya mara kwa mara ya makombora yake ya nyuklia.
Kwa mujibu wa taarifa zizlitolewa na baraza la Ulaya, atua hiyo imechukuliwa chini ya misingi ya maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Vikwazo hivyo ni pamoja na kuongezwa kwa watu 16 mashuhuri na mashiriki ya Korea-Kaskazini katika orodha ya vikwazo.
Umoja wa Ulaya uliweka vikwazo dhidi ya Korea-Kaskazini mwaka 2006 na kupiga marufuku kwa wawekeza wa Ulaya mwaka 2017 kuuzia mafuta Korea-Kaskazini.
No comments:
Post a Comment