Monday, January 8, 2018

8 January 2018,Watu kadha wanahofiwa kufa maji baada ya Mashua ya wahamiaji haramu kuzama baharini

Mashua iliokuwa na wahamiaji haramu kutoka barani Afrika 290 yazama katika bahari ya Mediterania.

Wahamiaji katika mashua hiyo walikuwa na lengo la kuvuka bahari ya Mediterania na kuengesha katika fukwe za Italia.

Miili ya wanawake miwili imeokotwa kandokando ya bahari huku taarifa zikifahamisha miili mingine bado haijapatikana.

Mmiliki wa mashua hiyo aliekuwa akiwasafirisha mahamiaji hao alijaribu kukimbia bila ya mafaanikio.

Kikosi cha uokozi kimefaulu kuwaokoa wahamiaji 250 huku zoezi la kuwaokoa wahamiaji wengine waliokosekana zikiendelea.

Watu  zaidi ya 120 000 walivuka bahari ya Mediterania mwaka 2017 kupitia Libya na kuegesha katika fukwe za Italia.

No comments: