Friday, January 5, 2018

5 January 2018,Pakistan yalipiza alichokisema Trump juu ya msaada unaotolewa nchini humo

Rais wa Marekani Donald Trump amekuwa akiandika ujumbe mbalimbali kupitia mtandao wake wa twitter.

Siku chache zilizopita,rais Trump aliandika katika twitter kuwa Marekani imekuwa ikitoa msaada kijinga kwa nchi ya Pakistan.
Pakistan nayo imesema kuwa historia imewafundisha kutoiamini Marekani mia kwa mia.

Waziri wa mambo ya nje wa Pakistan Khawaja Asif amesema kuwa Pakistan imekuwa ikijizatiti na kujitolea katika mambo mengi ili kuifurahisha Marekani lakini imeshindikana.

Kwa mujibu wa habari,waziri huyo amedai kuwa Pakistan imekuwa ikijaribu kuiridhisha Marekani licha ya kuwa ilikuwa ikiathirika kiuchumi.

Vilevile ameelezea matatizo nchi yake imekuwa ikipata kutokana na vikwazo vilivyowekwa na Marekani.
Hata hivyo Pakistan imeahidi kutojidhalilisha tena.

No comments: