Watu wasiopungua 40 wameripotiwa kufariki katika mashambulizi yaliotekelezwa katika kipindi cha siku 2 eneo la Guta Mashariki nchini Syria.
Mashambulizi yanaripotiwa kuendelea, jambo ambalo linakadiriwa kuwa idadi ya watu wanaofariki katika mashambulizi hayo yataongezeka.
Taarifa zafahaömisha kuwa jeshi la Assad limeendesha mashambulizi ya anga dhidi ya miji tofauti katika eneo la Gura Mashariki nchini Syria.
Maeneo yalioshambuliwa ni maeneo ambayo yalikuwa chini ya usimamizi wa mkataba wa kusitisha mapigano nchini Syria.
Mashambulizi hayo yamesababisha vifo vya watu wasiopungua 40.
Shukhuli za uokozi zinaeendelea na matumaini ya kuwapata watu walionaswa katika majumba yalioshambuliwa kwa mabomu bado ni makubwa.
Majeruhi walipelekwa katika hospitali zinazopatika karibu ya maeneo ya matukio kupewa matibabu.
No comments:
Post a Comment