Watu 13 wameripotiwa kufariki katika ajali iliotokea katika pwani ya Korea Kusini baada ya meli kugongwa na mashua ndogo ya wavuvi.
Katika ajali hiyo watu wengine wawili hawajulikani walipo huku kikosi cha kulinda pwani kikifahamisha kuwa kinaendesha shuhuli ya kuwatafuta.
Taarifa zizlitolewa na kituo cha habari cha Yonhap zimefahamisha kuwa mashua yenye uzito wa tani 9,8 imegonga meli yenye uzito wa tani 336 kusababisha kuzama kwake.
Mashua hiyo ya wavuvi ilikuwa na watu 22 ambapo 13 wamefariki na wengine bado wakitafutwa na kikosi chaa uokoaji.
No comments:
Post a Comment