Friday, December 15, 2017

15 December 2017,Mbunge wa CHADEMA ashangaza na kuleta gumzo leo hii...

Mbunge wa Chadema, Upendo Peneza amezua gumzo kwenye mitandao ya kijamii baada ya mbunge huyo kuitisha mkutano na waandishi wa habari bila kueleza atakachozungumza.

Peneza mbunge kutoka Mkoa wa Geita ameitisha mkutano huo kipindi ambacho kumekuwa na vuguvugu la wabunge kukikimbia chama hicho na kujiunga na CCM.

Mkutano huo umeitisha ikiwa ni siku moja kupita tangu mbunge wa Siha wa Chadema, Dk Godwin Mollel alipotangaza kuhamia CCM akiunga jitihada za Rais John Magufuli.

Akizungumza  leo Desemba 15, Peneza amesema ‘’nitakuwa na mkutano na waandishi,”

Wanahabari walipotaka kujua kama mkutano huo atautumia kutangaza kuhama, Peneza hakukubali wala kukanusha zaidi ya kusisitiza ‘’wewe njoo katika mkutano utaelewa nakwenda kuzungumza nini.”



Admit Mwananchi

No comments: