Thursday, November 9, 2017

9 November 2017,Watu kumi wameuawa nchini Afghanistan kutokana na matumizi mabaya ya anga ya Marekani

katika hujuma ya anga
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan UNAMA umesema mashambulizi ya anga ya hivi karibuni yaliyotekelezwa na ndege ya kivita ya Marekani yameua raia wasiopungua 10.

Vyombo vya habari nchini Afghanistan vimeripoti habari hiyo kwa kunukuu taarifa iliyochapishwa na UNAMA katika ukurasa wake rasmi wa mtandao wa kijamii wa Twitter inayosema kuwa: Kwa akali, raia 10 waliuawa katika mashambulizi ya anga ya ndege za US Novemba 4 katika mkoa wa Kunduz.

Hata hivyo Baraza la Mkoa wa Kunduz limesema ni raia 15 waliuawa katika mashambulizi hayo katika vijiji vya Gharaw Qeshlaq, Rajkia na Qatlam.
Serikali ya Kabul imesema hujuma hizo za anga ni sehemu ya operesheni ya US dhidi ya maficho ya kundi la kigaidi na kitakfiri la Taliban, katika wilaya ya Char Dara.

Mapema mwezi huu, Mkuu wa Baraza la Utekelezaji la Serikali ya Umoja wa Kitaifa nchini Afghanistan, Abdullah Abdullah aliwataka askari wa kigeni wanaoongozwa na Marekani waondoke nchini humo, akibanisha kuwa, raia wa Afghanistan wanapinga uwepo wa askari ajinabi nchini mwao.

Hadi sasa karibu askari elfu 14 wa kigeni wakiwemo askari elfu 11 kutoka Marekani, wapo nchini Afghanistan.

No comments: