Wahamiaji haramu 31 wafa maji na wengine 35 waokolewa baada ya mashua yao kuzama katika pwani ya Libya
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na polisi ya pwani ya Libya ni kwamba wahamiaji haramu 31 wamefariki na wengine 35 wamokolewa baada ya mashua yao kuzama nchini Libya.
Msemaji wa polisi ya kulinda pwani Libya kanali Ayub Qassem amefahamisha Jumamosi kuwa operesheni ya kuwaokowa wahamiaji hao ilifanyika katika eneo la Castelverde Mashariki mwa Tripoli.
Kanali huyo amefahamisha kuwa miongoni mwa watu waliookolewa walikuwemo watoto.
No comments:
Post a Comment