Mwenyekiti wa bodi ya mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF Anne Makinda ametoa wito kwa watanzania kujiunga kwenye mifuko ya bima ya afya ili kupunguza mahitaji ya gharama za matibabu pindi matatizo yanapojitokeza.
Makinda ametoa kauli hiyo mkoani Kigoma wakati akizungumza katika mahafali ya shule ya sekondari Mavuno iliyopo wilayani Kasulu ambapo pamoja na mambo mengine amesema bado watu wengi wanapoteza maisha kutokana na kushindwa kumudu gharama za matibabu jambo ambalo kupitia mifuko hiyo limerahisishwa.
Hii ni mahafali ya tatu katika shule ya Sekondari Mavuno iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
No comments:
Post a Comment