Friday, November 10, 2017

10 November 2017,Viongozi watawala barani Afrika watajwa kuingilia uhuru wa Tume za Chaguzi

Suala la machafuo yanayotokea baada ya chaguzi mbalimbali barani Afrika, ni kati ya mada zinazoendelea kujadiliwa na wenyeviti wa tume za uchaguzi kwenye nchi za Kiafrika katika mkutano wao ulioanza Akhamisi ya leo jiji Kigali, Rwanda.

Aidha suala la wanasiasa wanaowatumia vijana kwa ajili ya maslahi yao binafsi ya kisiasa, nalo limejadiliwa katika kikao hicho, ambapo wanasiasa wamekuwa wakiwatumia vijana katika kuibua vurugu na machafuko kwa lengo la malengo yao ya kisiasa.

Hata hivyo wenyeviti wa tume za chaguzi katika nchi za bara hilo wamesema kuwa hali hiyo imekuwa ikisababishwa na wanasiasa wenye maslahi binafsi ambao kwa kiasi kikuwa hutumia madaraka yao kuingilia uhuru na utendaji kazi za tume huru za uchaguzi.

No comments: