Wednesday, November 1, 2017

1 November 2017,Kiongozi wa upinzani kaskazini mwa Cameroon ahukumiwa jela miaka 25

Kiongozi wa chama cha upinzani kaskazini mwa nchi ya Cameroon, Aboubakar Siddiki amehukumiwa kwenda jela miaka 25 kwa makosa ya kuchochea uasi.

Shirika la haki za binadamu la Amnesty International limeikosoa mahakama ya kijeshi nchini Cameroon kwa kumhukumu kiongozi huyo miaka 25 jela kwa makosa ya uasi likidai hakuna ushahidi uliotolewa mahakamani kuchangia hukumu kama hiyo.

Aboubakar Siddiki alikamatwa mwaka 2014 baada ya kudaiwa kupanga njama za kuipindua serikali iliyo madarakani ya Rais Paul Biya.

No comments: