Saturday, October 7, 2017

7 October 2017, Kata 43 nchini kuchangua Madiwani Novemba 26 mwaka huu

Mwenyekiti wa NEC Jaji Semistocles Kaijage, amesema kuwa uchaguzi huo unafanyika kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo baadhi ya madiwani kufariki dunia, kujiuzulu, kutohudhuria vikao na wengine ushindi wao kutenguliwa na Mahakama.

Jaji Kaijage amesema tume imetangaza kufanyika kwa uchaguzi huo mdogo, baada ya waziri mwenye dhamana ya serikali za mitaa kuitaarifu tume uwepo wa nafasi wazi za madiwani katika kata hizo 43 zilizoko katika halmashauri mbalimbali 36 na mikoa 19 ya Tanzania Bara.

Aidha  Kaijage ameainisha kwamba kifungu cha 13 (1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya. 292 kinampa mamlaka waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa kuitarifu tume kuhusu kuwepo kwa uchaguzi huo mdogo wa madiwani.

Amefafanua kuwa baada ya kupokea taarifa hiyo na kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 13(3) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa; Sura ya 292, Tume ya taifa ya uchaguzi ina wajibu wa kuitisha na kuendesha Uchaguzi mdogo katika Kata hizo.

“Hivyo, ninapenda kuchukua nafasi hii kutoa taarifa kuwa tume imepanga kuendesha uchaguzi mdogo katika Kata 43 tarehe 26 Novemba, 2017,” alisema Jaji Kaijage.

Amesema ratiba ya mchakato wa uchaguzi huo itaanza Oktoba 26 ambapo kutafanyika uteuzi wa wagombea udiwani na kampeni za uchaguzi huo mdogo zitaanza Oktoba 27 na kumalizika Novemba 25.

Jaji Kaijage aliema Vyama vya Siasa, Wadau wote wa Uchaguzi na Wananchi wanakaribishwa kwa ajili ya kushiriki kwenye uchaguzi huo utakaozingatia ratiba iliyoainishwa hapo juu.

Alitoa mwito kwa vyama vya Siasa na Wadau wote wa Uchaguzi kuzingatia matakwa ya Katiba, Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (Madiwani) za mwaka 2015, Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015 pamoja na maelekezo yote yaliyotolewa au yatakayotolewa na Tume wakati wote wa Uchaguzi mdogo.

Kata ambazo zitashiriki kwenye uchaguzi huo ni kama ilivyoanishwa kwenye jedwali hapa chini:

Na MKOA HALMASHAURI KATA

1. ARUSHA

Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Musa

Halmashauri ya Jiji la Arusha Muriet

Halmashauri ya Wilaya ya Meru Ambureni

Halmashauri ya Wilaya ya Meru Ngabobo

Halmashauri ya Wilaya ya Meru Maroroni

Halmashauri ya Wilaya ya Meru Leguruki

Halmashauri ya Wilaya ya Meru Makiba

Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Moita

2. 2 DAR ES SALAAM

Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Mbweni

Halmashauri ya Manispaa ya Temeke Kijichi

Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Saranga

3. DODOMA Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Chipogolo

4. GEITA

Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’wale Bukwimba

Halmashauri ya Wilaya ya Geita Senga

5. IRINGA

Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Kitwiru

Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo Kimala

6. KILIMANJARO

Halmashauri ya Manispaa ya Moshi Bomambuzi

Halmashauri ya Wilaya ya Hai Mnadani

Halmashauri ya Wilaya ya Hai Machame Magharibi

Halmashauri ya Wilaya ya Hai Weruweru

7. LINDI

Halmashauri ya Manispaa ya Lindi Chikonji

Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mnacho

8. MANYARA Halmashauri ya Wilaya ya Hanang’ Nangwa

9. MBEYA Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Ibighi

10. MOROGORO

Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Kiloka

Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Sofi

11. MTWARA

Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Milongodi

Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani Reli

Halmashauri ya Mji wa Masasi Chanikanguo

12. MWANZA

Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Kijima

Halmashauri ya Jiji la Mwanza Mhandu

13. RUKWA Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga Sumbawanga

14. 14 RUVUMA Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru

No comments: