Thursday, October 5, 2017

5 October 2017, Hawa ndio watu wanaogopa kifo zaidi duniani

KIFO:Watu wengi duniani huogopa kufa lakini kwa Wazayuni imekuwa zaidi  ,simanzi hutokea,majonzi upweke  pale mtu anapofiwa

Maranyingi hali hii huwakumba wale wenye mahusiano ya karibu na aliyefariki (MAREHEMU) ,kwa watu wasio na ukaribu na tukio hilo huona kawaida ila fiwa uone adha iliyoje

Kituo kimoja wa Kizayuni kimetangaza data zilizotolewa na kituo cha kukusanya takwimu za hoteli za kimataifa na kukiri kuwa, Wazayuni ni watu nambari moja kwa woga na kuogopa kifo duniani.

Shirika la habari la ISNA limeunukuu mtandao wa Kizayuni wa "Israel Today" ukisema katika ripoti yake kwamba makumi ya watalii Wazayuni wamebadilisha safari zao kuelekeza Korea Kusini na pia wameghairi kuchukua vyumba walivyokuwa wamewekeza katika hoteli za Korea Kusini kwa kumuogopa Kim Jong-un, kiongozi wa Korea Kaskazini.

Kituo hicho cha Kizayuni vile vile kimesema kuwa, kuna upungufu wa asilimia 33 ya watalii wa Israel huko Korea Kusini huku idadi ya watalii kutoka Japan ikipungua kwa asilimia 17 na watalii kutoka Russia wamepungua kwa asilimia 16 nchini humo.

Ripoti hiyo imeongeza kuwa, Wazayuni wameghairi kuchukua vyumba walivyowekeza katika hoteli za Korea Kusini katika hali ambayo hadi hivi sasa watalii kutoka Marekani, Ulaya, China, Canada na Australia wamejaa katika hoteli hizo za Korea Kusini.

No comments: