Tuesday, October 17, 2017

17 October 2017, Mabudha hawajaacha kuwaua Waislamu wa Rohingya

Licha ya kuendelea kulaaniwa na kutolewa radimali kubwa kutoka pembe mbalimbali za dunia kuhusiana na jinai za jeshi na Mabudha magaidi wa Myanmar kuwalenga Waislamu wa jamii ya Rohingya nchini humo, bado wimbi la mauaji na jinai kubwa dhidi ya watu hao zinaendelea kila siku.

Katika ripoti mpya zilizotolewa na vyombo vya habari, maelfu ya Waislamu wa Rohingya wameendelea kuingia nchini Bangladesh kwa wingi kutokana na kushtadi mashambulizi ya jeshi la serikali kwa kushirikiana na Mabudha magaidi, kunyimwa chakula na kuchomwa moto makazi yao nchini Myanmar.

Waislamu hao hawana njia nyingine ghairi ya kuwa wakimbizi ili kunusuru maisha yao.

Pritam Kumar Chaudhry, Mkuu wa Shirika la Huduma za Kijamii nchini Bangladesh ameelezea uwepo wa watoto elfu 14 wa Rohingya wasio na uangalizi katika kambi za wakimbizi hao eneo la Cox's Bazar na kwamba hali yao ya kimaisha ni mbaya sana.

Gazeti la Bangkok Post limeandika kuwa, Waislamu wa Rohongya walioko katika mpaka wa Myanmar na Bangladesh wanakabiliwa na hali mbaya kukiwemo kushambuliwa na tembo ambazo zimekuwa zikivamia kambi zao na kusababisha mauaji.

Hayo yanajiri katika hali ambayo mamia ya watu wa jamii hiyo ya Rohingya wameendelea kuzama maji katika mto ulio mpakani kati ya Bangladesh na Myanmar.

Polisi ya Bangladesh imetangaza kuwa, katika tukio la hivi karibuni kabisa zaidi ya watu 40 wametoweka na kufanikiwa kupata miili minane ya Waislamu hao wa Rohingya, kufuatia mtumbwi waliokuwa wakitumia kuzama maji.

Hayo yanajiri katika hali ambayo, Jumuiya ya Mabunge imelaani mauaji na jinai dhidi ya Waislamu Warohingya nchini Myanmar katika kikao chake huko Saint Petersburg nchini Russia mkutano ambao umefanyika kwa ubunifu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambapo pia imetaka kuchukuliwa hatua kali kuzuia jinai hizo.

No comments: