Wednesday, October 11, 2017

11 October 2017,Wamiliki halali wa viwanja Tabora kurudishiwa

Naibu waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula amemuagiza mkurugenzi wa Manispaa ya Tabora John Bosco kuvirejesha viwanja  kwa wamiliki halali mbalimbali vikiwamo viwanja sita vya Chama Cha Mapinduzi ambavyo vimemilikishwa kwa watu binafsi.

Mabula ametoa agizo hilo kufuatia watalaam wa ardhi waliokiuka maadili kwa kugawa kiwanja moja kwa zaidi ya mtu mmoja na amewataka kutoa maelezo ya kina kuhusiana na ukiukwaji huo wa maadili ya kazi.

Pia amesisitiza kwa taasisi mbalimbali kuweka alama za mipaka katika viwanja wanavyovimiliki.

Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri ametoa maagizo ya kuchukuliwa hatua kwa watumishi waliogawa viwanja

No comments: