Tuesday, October 10, 2017

10 October 2017,Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa wauawa Congo

Wanajeshi wawili wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa MONUSCO wameuawa katika shambulizi lililolenga kambi yake Mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Wanajeshi wengine kadhaa wameripotiwa kujeruhiwa katika shambulizi hilo linaloshukiwa kutekelezwa na waasi kutoka nchini Uganda.

Taarifa hiyo ilitolewa na ofisi za Umoja wa Mataifa Jumatatu .

Kambi ya Monusco ilioshambuliwa inatambulika kwa jşna la Mamundioma Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

No comments: