Saturday, September 9, 2017

9 September 2017, Azam,Simba wachoshana nguvu

Azam FC leo imecheza dhidi ya Simba katika mchezo wao wa LigiKuu Tanzania bara msimu wa 2017/2018 dhidi ya Simba katika uwanja wa Chamazi lakini game haikufanikiwa kupata mbabe na kulazimika kwa sare tasa ya 0-0, huo ulikuwa ni mchezo wa pili waLigi Kuu kwa timu zote mbili.

Mchezo wa leo wa Azam FC dhidiya Simba unakuwa ni mchezo wao wa 19 kukutana kwa timu hizo katika Ligi Kuu toka walipokutana October 4 2008 na Azam kuibuka na ushindi wa magoli 2-0, kwa ujumla Simba kaifunga Azam FC katika Ligi mara 8 na kupoteza mara 5 na sare wametoka mara sita.

Kwa matokeo hayo sasa Azam FC na Simba zote zinafungana kwa kuwa na point nne kila mmoja katika msimamo wa Ligi Kuu wakitofautiana magoli, Simba sasa atacheza game yake ya tatu dhidi ya Mwadui FC katika uwanja wa Uhuru wakati Azam FC wao watacheza na Kagera Sugar katika uwanja wao wa Chamazi.

No comments: