Zaidi ya wakimbizi 60 kutoka jamii ya Rohingya wafariki baada ya mashua yao kuzama wakijaribu kukimbia mauaji Myanmar
Mashua ilikuwa ikiwasafarisha wakimbizi kutoka jamii ya Rohingya imeripotiwa kuzama n kusababisha vifo vya watu zaidi ya 60.
Msemaji wa shirika la kimataifa la wahamiaji Joel Millman amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva kuwa mashua ilikuwa ikiwasafirisha waislamu wa jamii ya Rohingya waliokuwa wakikimbia mauaji Myanmar imezama na kusabaisha maafa hayo.
Mashua hiyo imeripotiwa kuzama katika usiku wa Alhamisi.
Taarifa zinafahamisha kuwa watu wengine zaidi ya 40 hawajulikani walipo.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na watu walionusurika katika ajali hiyo, katika mashua hiyo kulikuemo watoto zaidi ya 30.
No comments:
Post a Comment