Baadhi ya wasafiri na wakazi visiwani Zanzibar wameshindwa kusafiri na kwenda kwenye shughuli zao za kila siku kutokana na tatizo la uhaba wa mafuta ya petrol na dizeli lililopo visiwani humo kwa siku tatu mfulilizo.
Kwa mujibu wa TBC Mjini Unguja baadhi ya vituo vya mafuta vimefungwa huku vingine vikiwa na msongamano mkubwa wa wananchi wanaotaka kupata huduma hiyo.
Kufuatia hali hiyo baadhi ya vijana walionunua mafuta kwenye madumu mapema wanauza lita moja ya mafuta ya petrol shilingi elfu nne badala ya elfumbili.
No comments:
Post a Comment