Monday, September 18, 2017

18 September 2017,TANESCO:Zaidi ya nguzo za umeme 130 na vifaa nya umeme vimeibwa Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya

Zaidi ya nguzo za umeme 130 na vifaa vingine vya umeme mali ya Shirika la Umeme nchini -TANESCO Mkoa wa Mbeya na Wakala wa Umeme Vijijini –REA vimeibwa katika Vijiji vya Ilalabwe, Ngana, Iponjola Wilayani Rungwe.
Afisa Usalama TANESCO Mkoa wa Mbeya, Kembe Sabini amesema wamebaini wakandarasi waliopewa zabuni ya kusambaza umeme vijijini Wilayani Rungwe nao wanahusika na wizi huo na kuwaunganishia umeme wananchi ambao hawamo kwenye orodha ya kuunganishiwa nishati hiyo.
Mkoa wa Mbeya unadaiwa kukumbwa na wimbi la vishoka katika kipindi hiki ambacho serikali imekusudia kufikisha nishati ya umeme vijijini kwa utaratibu.
Wakala wa Umeme Vijijini -REA anatekeleza mradi wa umeme awamu ya tatu, ambapo Mkoani MBEYA vijiji 196 vinarajiwa kupelekewa huduma hiyo ya umeme awamu hiii ya tatu


No comments: