Jeshi la Polisi Mjini Unguja linawashikilia watu ishirini wanaosadikiwa kujihusisha mapenzi ya jinsia moja.
Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa polisi Mkoa wa Mjini Magharib Hassan Nassir amesema watu hao wamekamatwa wakati wakipatiwa mafunzo ya namna ya kuzitambua haki zao yaliyokuwa yakitolewa na taasisi iliyotambulika kwa jina la Bridge Initiative.
Kamanda Nassir amesema Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi na sheri zitachukuliwa dhidi ya watu wote wanaojishughulisha na vitendo hivyo.
Aidha Kamanda Nassir ametoa wito kwa wazazi na walezi kuwa karibu na vijana wao ili kuwanusuru kujiingiza katika taasisi zinazotoa mafunzo kinyume na maadili.
No comments:
Post a Comment