Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela ameanza kukabiliana na migogoro ya ardhi katika Jiji la Mwanza kwa kuwakutanisha maafisa ardhi na wananchi katika mikutano ya hadhara zikiwa ni jitihada za kutatua kero ya ardhi ambayo imeligubika jiji hilo kwa muda mrefu.
Akizungumza na mamia ya wananchi kutoka katika Manispaa ya Ilemela na Jiji la Mwanza, Mongella ameweza kutafuta suluhu ya migogoro hiyo iliyosababisha baadhi ya wazee kupata haki zao ambazo wamekuwa wakifuatilia kwa zaidi ya miaka 20.
Katika mikutano hiyo Mongella amefuatana na wataalamu wa kitengo cha ardhi katika Manispaa ya Ilemela na Jiji la Mwanza kwa ajili ya kutoa majibu ya kero mbalimbali za ardhi zinazowakabili wananchi.
No comments:
Post a Comment