Thursday, September 14, 2017

14 September 2017, IGP SIRRO :Wananchi watoe ushirikiano kwa Jeshi la Polisi

Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro, alizungumzia suala la Lissu kupigwa risasi akiwataka wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha ili kufanikisha kuwatia mbaroni wahalifu waliohusika.

“Naomba wananchi wasidanganywe kwenye suala zima la siasa na vitu vingine, huwa nasema siku zote, kama hakuna amani na usalama siasa haiwezi kupata nafasi, tukio hili limetokea, tunapeleleza na tupo makini na hili tukio.

“Kwa sasa tumeongeza vikosi vya upelelezi Dodoma, wale waliofanya lile tukio ni lazima tutawakamata, ila upelelezi huu unaweza kuzaa matunda mazuri zaidi endapo wananchi watatupa ushirikiano wa kutosha,” alisema IGP Sirro.

No comments: