Wednesday, September 13, 2017

13 September 2017, Kenyatta kutumia bunge kumuondoa Odinga iwapo atashida uchaguzi

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta asema kuwa atatumia bunge kumuonda Raila Odinga iwapo atashinda katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

Mahakama ya juu nchini Kenya ilibatilisha matokeo ya uchuguzi uliofayinga Agosti mwaka  huu baada ya Raila Odinga kufikisha malalamiko yake mbele ya mahakama kuwa uchaguzi ulikuwa si wenye haki na kuonekana kuwa wenye dosari nyingi.

Mahakama ya juu na tume ya uchaguzi ilifuta matokeo ya uchaguzi na kutangaza kuwa uchaguzi utarejelewa ifikapo Oktoba 17.

Rais Uhuru Kenyatta amesema kuwa bunge litamtoa madarakani Raila Odinga iwapo atashinda katika uchaguzi.

Wabunge wengi katika baraza la bunge la Kenya ni wanachama kutoka katika chama cha Jubilee.

No comments: