Rais John Magufuli amemteua Profesa Ibrahim Juma kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania.
Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu Jijini Dar es salaam imesema uteuzi huo unaanza leo.
Kabla ya uteuzi huo Profesa Ibrahim Juma alikuwa akikaimu nafasi hiyo.
Profesa Ibrahim Juma amechukua nafasi ya Jaji Mstaafu Mohamed Chande Othman ambaye amestaafu.
Profesa Ibrahim Juma ataapishwa kesho saa nne asubuhi Ikulu Jijini Dar es salaam .
No comments:
Post a Comment