Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imezifuta timu mbili kutoka daraja la pili kwa kushindwa kukamilisha usajili wa vilabu vyao katika kuelekea michuano ya Ligii kwa msimu wa mwaka 2017/2018.
Hayo yamenyambulishwa na taarifa iliyotolewa na Afisa habari wa (TFF), Alfred Lucas na kusema timu hizo zimeshindwa kujisajili, kuingiza majina ya wachezaji pamoja na kuingiza viongozi wa benchi la ufundi kwenye mfumo wa mtandao 'Transfer Matching System' (TMS) ni za Ligi Daraja la Pili (SDL) ambazo ni Pepsi ya Arusha na Bulyanhulu ya Shinyanga.
"Kwa msingi huo, timu hizo za Pepsi na Bulyanhulu zimejitoa kushiriki ligi kwa msimu wa 2017/2018 na zinashushwa daraja hadi ligi ya Wilaya kuanza upya kutafuta nafasi za juu kupanda daraja", amesema Alfred.
Pamoja na hayo, Alfred amesema tayari majina ya timu 62 kati ya 64 zilizokamilisha usajili wake wamezibandikwa katika mabao ya matangazo ya Shirikisho hilo kwa lengo la kuwapa fursa timu zote kukagua majina ya wachezaji wa kila timu ili kuona kama kuna klabu au mchezaji amefanya udanganyifu wa kusajili wa timu zaidi ya moja, ziweze kuona.
"Kama kutakuwa na dosari katika timu hizo, TFF imefungua milango ya kupokea pingamizi la usajili wa wachezaji hao kuanzia leo Agosti 8 hadi Jumatatu Agosti 14 mwaka huu saa 10.00 jioni", amesisitiza Alfred.
Kwa upande mwingine, Alfred amesema Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji inatarajiwa kuwa na kikao ama Agosti 16 au 17, mwaka huu kwa lengo la kupitia mapingamizi hayo pamoja na usajili wa timu za Ligi Kuu Tanzania Bara, Usajili wa timu za Daraja la Kwanza na Pili, utapitiwa baadaye mwezi huu.
No comments:
Post a Comment