Rais Dkt. Joh Magufuli amemtaka Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage aache uoga wa kuvifuta viwanda na kuwanyanganya ambao wameshindwa kuvindeleza.
Rais Dkt. Magufuli ametoa agizo hilo leo Mkoani Tanga wakati akizindua kiwanda cha saruji kiitwacho Kilimanjaro ambacho kipo ndani ya mkoa huo.
"Nimpongeze Mh. Waziri wa Viwanda Charles Mwijage kwani kazi zake nyingi ni 'excellent' lakini tatizo lake ni uoga tu wakufukuza kwenye hilo ndiyo unanikwaza. Viwanda ambavyo havifanyi kazi vipo tu kwa nini havifutwi ?, Waziri Mwijage unamuogopa nani wakati mimi ndiye niliyekuteua. Nimekuelezea tukiwa ofisini tukiwa kwenye 'cabinet' na hadharani kote hujanisikia, unataka nikuelekeze nikiwa kaburini ?", amesema Rais Magufuli.
Pamoja na hayo, Rais Magufuli ameendelea kwa kusema "Tanzania tuna viwanda 197 ambavyo vimelala havifanyi kazi hapa Tanga mmesema vipo 12 vimesinzia kabisa, futa vyote. Nakuagiza tena, fungia viwanda vyote visivyoendelezwa wakitupeleka Mahakamani tutajua namna ya kupambana nao, sheria zipo", amesisitiza Rais Magufuli.
Katika hatua nyingine, Rais Dkt. Magufuli ameridhia ombi la Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu la kutanua uwanja wa ndege wa mkoa wa Tanga ili ziweze kutua ndege nyingi zaidi na kubwa tofauti na sasa ambapo zinatua ndege nne tu na ndogo.
No comments:
Post a Comment