Sunday, August 20, 2017

20 August 2017, Namna ya kubadili macho madogo kuwa makubwa

JICHO ni kiungo muhimu katika mwili wa binadamu na ndiyo maana watu huchunga sana wasiharibikiwe macho, maana ndiyo taa ya mwili.

Pamoja na kuwa kuna viungo vingine kwa ajili ya ufahamu wa mtu, lakini linaongoza kwa matumizi ya ufahamu kwa watu wengi. Pamoja na umuhimu huo, lakini macho pia ni sehemu ya pambo la mwili (hasa kwa wanawake).

Nasema hivyo kwa sababu wanawake wengi hupenda kuyapamba macho yao na hivyo kuonekana wakivutia zaidi. Lakini kuna macho ya aina mbili, makubwa na madogo.

Kwa kawaida mwanamke anapokuwa na macho makubwa huwa na mvuto wa kipekee.

Lakini pia mwanamke mwenye macho madogo anaweza kuyapamba macho yake na yakaonekana makubwa.

Katika makala ya leo tutaangalia mbinu ya kufanya ili mtu uonekane mwenye macho makubwa hata kama asili yako ni macho madogo.

Mahitaji: Wanja wenye rangi iliyokolea na rangi ya kawaida, maskara, pamba kiasi na kope za bandia. Njia: Paka wanja usiokolea kwenye kingo za nje za kope zako na si eneo la ndani.

Ni vema kuanza na wanja ambao haujakolea sana na baadaye kupaka wanja uliokolea ili kuhakikisha unapendeza zaidi. Unaweza kupaka wanja mpaka nje kidogo ya kingo za jicho, yaani upande wa kulia na kushoto. Baada ya hatua hiyo, bandika kope bandia kwa uangalifu.

Kumbuka kwamba kope bandia (hasa zinapokuwa na urefu wa kutosha) hufanya mwanamke aonekane mwenye macho makubwa.

Hatua hiyo ikimalizika, mwanamke anaweza kupaka maskara ya kutosha ambayo itanyanyua kope zaidi na kuonekana mrembo. Kumbuka kwamba kama huwezi kufanya jambo hilo wewe mwenyewe, unatakiwa kuomba mtu akusaidie ili kuwa na matokeo mazuri.

Admit  Ndaya Mgoyo

No comments: