Kiongozi wa upinzani nchiini kenya Raila Odinga ametangaza kuwa muungano wa NASA katika uchaguzi utawasilisha kesi katika mahakama kupinga matokeo ya uchaguzi yaliomtangaza rais Uhuru Kenyatta mshindi katika uchaguzi uliofanyika Juma lililopita nchini humo.
Raila Odinga amesema kuwa ni vema kwa muungano huo kufichua uovu na udanganyifu uliotendeka katika zoezi zima la kupiga kura katika uchaguzi mkuu.
Raila Odinga anatuhumu tume ya uchaguzi ya taifa IEBC kuvuruga matokeo ya uchaguzi kwa madai ya kudukuliwa na kumpa ushindi rais Uhuru Kenyatta.
Hayo Raila Odinga alizungumza kwa waandishi wa habari Lavington mjini Nairobi.
No comments:
Post a Comment