Wednesday, August 16, 2017

16 August 2017, TP Mazembe FC yatinga robo fainali

Timu ya soka ya TP Mazembe FC imetinga hatua ya robo fainali ya mashindano ya Rwakatare Cup 2017 baada ya kuifunga Mkamba B kwa mabao 2-0 katika mashindano yanayoendelea kutimua vumbi vituo saba kwenye Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro.

Mashindano hayo yanaendelea kuchezwa kwenye vituo saba vya yanashirikisha jumla ya timu 80 ambazo kila kituo itatoa mshindi wa kwanza na pili ili kupata timu 14 za kuwania ubingwa wa Rwakatare Cup 2017.

Msimamizi wa kituo cha Mkamba, Clarence Msavila alisema kuwa kituo hicho tayari timu nane zimefuzu kucheza robo fainali lakini TP Mazembe ililazimika kupambana ili kupata nafasi katika mchezo wake wa mwisho kwa kupata ushindi.

Admit Mwananchi

No comments: