Ripoti zinaonyesha kuwa janga la njaa limesababisha idadi ya waliopoteza maisha kuongezeka kwa milioni 1.8 DRC.
Kwa mujibu wa habari,Umoja wa Mataifa umesema kuwa kati ya sababu zilizosababisha kuongezeka kwa njaa ni kuzidi kwa migogoro na wahamiaji nchini humo.
Ukilinganisha idadi ya waliopoteza maisha kutokana na njaa mwaka jana,na idadi iliyoripotiwa mwezi Juni mwaka huu,ni wazi kuwa watu milioni 1.8 zaidi wamefariki na kusababisha idadi kamili kuwa milioni 7.7.
Mapigano na fujo ambazo zimekuwa zikiendelea DRC zimekuwa sababu mojawapo ya wakulima kutojishughulisha kikamilifu katika uzalishaji wa vyakula.
Magonjwa kama Surua na kipindupindu yamechangia kuhatarisha maisha ya wananchi nchini humo.
Hata hivyo UN imesisitiza kuwa hali itazidi kuwa mbaya endapo nchi hiyo haitopewa msaada wa dharura.
Chanzo trt swahili
No comments:
Post a Comment