Mtoto wa miaka tisa ni kati ya 24 waliouawa katika maandamano dhidi ya uteuzi wa rais Uhuru Kenyatta katika uchaguzi mkuu Kenya.
George Mwangi aliuawa na risasi Mathare,sehemu ambayo ni ngome ya kiongozi wa upinzani Raila Odinga siku ya Jumamosi.
Ripoti zinaonyesha kuwa sehemu kama Mathare na Kawangware mjini Nairobi na alipozaliwa bwana Odinga Kisumu ndio penye fujo zaidi Kenya nzima.
Kumekuwa na mzozano mkubwa kati ya raia na polisi toka kutangazwe kwa matokeo nchini humo.
Kwa mujibu wa habari,hakuna aneju kilichokuwa kinaendelea hasa katika usiku baada ya kutangazwa matokeo lakini watu wamepoteza maisha ikiwemo maafisa polisi.
Uhuru Kenyatta ametangazwa kama mshindi wa uchaguzi mkuu Kenya uliofanyika Agosti 8.
No comments:
Post a Comment